Lugha Nyingine
Kampuni ya maua ya Kenya yajaa matumaini kwa Maonesho ya Uagizaji Bidhaa ya China huku soko la China likivutia (7)
Mfanyakazi wa Karen Roses akichuma maua kwenye banda la kilimo cha kisasa huko Nairobi, Kenya Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Wang Guansen) |
Nairobi -- Ikipatikana sehemu za kaskazini za Nairobi, Kenya, Karen Roses, shamba la maua la kiasili, linajulikana kipekee kwa mimea yake iliyostawi kijani na vibanda vya kilimo cha kisasa vilivyopangwa vizuri, ambako aina mbalimbali za maua ya waridi tayari yako katika hali ya kuchanua.
Karen Roses imekuwa katika biashara ya maua ya kukatwa kwa zaidi ya miongo mitatu, ikiuza bidhaa zake kwenye masoko ya ndani na kimataifa, likiwemo soko la China.
Calvine Emadau, meneja wa biashara wa Karen Roses, amesema kwenye mahojiano na shirika la habari la China, Xinhua kuwa, Maonyesho yajayo ya saba ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yaliyopangwa kufanyika kuanzia Novemba 5 hadi 10, yatakuwa wakati muhimu kwa kampuni hiyo ya maua kupanua uwepo wake katika soko la China.
Ikiwa mwonyeshaji bidhaa wa mara ya kwanza, Karen Roses itaonesha baadhi ya bidhaa zake kuu kwenye maonesho hayo, zikiwemo kahawa na maparachichi, sambamba na ofa zake za maua.
“Tunaamini China ni soko la fursa zisizo na kikomo. Tulianza na China miaka mitano iliyopita; tumekuwa tukikua na kuamini hilo kweli ni soko zuri kwetu,” amesema Emadau.
Maonesho ya CIIE mwaka huu yatatoa kwa kampuni za upandaji maua za Kenya fursa ya kipekee ya kujua zaidi kuhusu soko la China, kujadiliana makubaliano ya uagizaji bidhaa, na kuanzisha ushirikiano wa biashara unaodumu, amesema Emadau.
Ili kuingia vizuri zaidi kwenye soko kubwa la China, Emadau amesema Karen Roses imepanga mkakati wake wa biashara ili kukidhi matarajio ya wateja.
Wateja wa maua wa China wana hulka ya kupendelea rangi nyororo, wakiendana na mwelekeo katika tasnia ya fasheni, ikiifanya Karen Roses kupanda aina mbalimbali za maua ya waridi kama vile “Spray Roses”, Emadau amesema, akiongeza kuwa soko la China pia linaweka mkazo kwenye udhibiti wa wadudu na kampuni hiyo imekuwa mara kwa mara ikiongeza viwango vyake vya uuaji wadudu kwa maua ya waridi yanayouzwa China.
Kwenye mkutano wa kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing Septemba 4 hadi 6, China iliahidi kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za kilimo za Afrika. Katika CIIE ijayo, kampuni za mazao ya kilimo za Afrika kama vile Karen Roses zinatumai kuonesha zaidi bidhaa zenye ubora wa juu kwa wateja tarajiwa, hatimaye kutanua mikondo yao ya mapato, amesema Emadau.
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma