

Lugha Nyingine
Kikosi cha Majini cha Jeshi la China chafanya zoezi la manoari mbili za kubeba ndege za kivita kwa mara ya kwanza (5)
![]() |
Manoari mbili za Liaoning na Shandong za China za kubeba ndege za kivita zikifanya zoezi la pamoja kwa mara ya kwanza katika Bahari ya Kusini ya China mwishoni mwa Oktoba 2024. (Picha na Sun Xiang/Xinhua) |
QINGDAO - Manoari mbili za Liaoning na Shandong za China za kubeba ndege za kivita zimefanya zoezi la pamoja kwa mara ya kwanza katika Bahari ya Kusini ya China, kwa mujibu wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).
Likilenga kuongeza uwezo jumuishi wa mapambano ya kivita ya manoari za kubeba ndege za kivita, zoezi hilo ni sehemu ya mafunzo ya kawaida ya manoari ya Liaoning baharini, ambayo yalihitimishwa hivi karibuni.
Mafunzo hayo yaliendeshwa katika bahari zikiwemo Bahari ya Manjano, Bahari ya Mashariki ya China na Bahari ya Kusini ya China, yakihusisha mafunzo ya aina mbalimbali chini ya hali halisi ya mapigano ya kivita, kikosi hicho kimesema.
Liaoning, manoari ya kwanza ya kubeba ndege za kivita ya China, ilikabidhiwa rasmi kwa Kikosi cha Majini cha PLA mwezi Septemba, Mwaka 2012.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma