

Lugha Nyingine
Mradi mpya wa umeme wenye nguvu zaidi waanza kufanya kazi kaskazini mwa China (3)
HOHHOT - Mradi wa kuzalisha umeme wenye voti kubwa wa kilovolti 1,000 (UHV) wa Zhangbei-Shengli umeanza kufanya kazi rasmi Alhamisi, ukiunganisha rasilimali za nishati safi kaskazini mwa China na mikoa yenye nguvu kiuchumi kama vile eneo la Beijing-Tianjin-Hebei.
Mradi huo unatarajiwa kusambaza umeme wa kutosha kwa kaya milioni 19 kwa mwaka -- kila mwaka kutoka eneo la Xilin Gol la Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China na Zhangjiakou katika Mkoa wa Hebei hadi eneo la Beijing-Tianjin-Hebei, mikoa ya Shandong na Jiangsu, na mikoa mingine.
Mradi huo unatumia teknolojia ya UHV kwa mara ya kwanza kuunganisha kituo cha nishati safi kaskazini mwa Hebei na mashamba ya upepo katika eneo la Xilin Gol, ukiongeza uwiano wa nishati mpya katika njia za upitishaji umeme wenye voti kubwa na kuongeza matumizi ya umeme wa kijani kwenye maeneo ya watumiaji wa mwisho wa umeme wa gridi ya taifa ya China, hivyo kuhimiza kuhamia kwenye nishati safi na yenye kutoa kaboni chache.
Mradi huo pia unatatua kwa ufanisi zaidi kuongezeka kwa mahitaji ya umeme katika mikoa inayopokea umeme huo.
China iko mstari wa mbele kiteknolojia katika uzalishaji wa nishati mpya, usambazaji wa umeme wa UHV, mkondo nyumbufu wa moja kwa moja wa moja wa usambazaji umeme na katika kuifanya mifumo ya umeme kuwa ya kidijitali, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Uunganishaji na Ushirikiano wa Nishati, ambalo ni shirika lisilo la faida la kimataifa lenye makao yake makuu mjini Beijing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma