Maafisa na wa wasomi wa Ethiopia wasifu mchango wa Huawei katika kuwezesha vijana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2024
Maafisa na wa wasomi wa Ethiopia wasifu mchango wa Huawei katika kuwezesha vijana
Dereje Engida, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Addis Ababa, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi tuzo za kutambua mafanikio ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Ethiopia katika fainali za kitaifa, kikanda na kimataifa za Shindano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) la Huawei 2023/2024, ambayo pia ni ya uzinduzi wa awamu inayofuata ya shindano hilo kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025, mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 31 Oktoba 2024. (Xinhua/Habtamu Worku)

ADDIS ABABA - Maafisa na wasomi wa Ethiopia wameipongeza kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei kwa "thamani yake ya kipekee" katika kutoa ujuzi na uzoefu muhimu wa kivitendo kuhusu teknolojia za kisasa za hali ya juu kwa vijana wa Ethiopia.

Wametoa pongezi hizo jana Alhamisi kwenye hafla ya kuwatunuku wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Ethiopia katika fainali za kitaifa, kikanda na kimataifa za Shindano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) la Huawei 2023/2024, ambayo pia ni ya uzinduzi wa awamu inayofuata ya shindano hilo kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Akihutubia hafla hiyo, Dereje Engida, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Addis Ababa (AASTU), amesema kushiriki kwa Huawei katika kujenga uwezo nchini Ethiopia kwa ujumla na ushirikiano wake na chuo kikuu hicho "vinaleta mageuzi katika mustakabali wa teknolojia nchini Ethiopia."

Amesema Akademia ya TEHAMA ya Huawei, moja ya akademia kubwa duniani kote katika nyanja hiyo, imeongeza kasi katika kuwezesha vijana wa Ethiopia kwa maendeleo ya hivi karibuni ya kiteknolojia.

Wanafunzi zaidi ya 1,100 wa AASTU wamejiunga na jukwaa la akademia ya TEHAMA ya Huawei, na wanafunzi zaidi ya 3,000 wameshiriki katika programu za uthibitishaji za Huawei, mashindano ya TEHAMA, na mpango wa kampuni hiyo "Mbegu za Siku za Baadaye".

Zelalem Assefa, afisa mtendaji mkuu wa TEHAMA na Elimu ya Kidijitali katika Wizara ya Elimu ya Ethiopia, amepongeza dhamira za maana za Huawei kwa fursa za ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu nchini Ethiopia.

Assefa amesisitiza zaidi mchango muhimu wa mipango ya Huawei katika kujenga uwezo kwenye suala la kuhamasisha fikra na ujuzi wa kijasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wa Ethiopia.

Kwa kutambua vipaji vya kipekee vya wanafunzi wa vyuo vikuu kwa mafanikio yao katika ngazi za kitaifa, kikanda, na kimataifa za awamu ya ya 2023-2024 ya shindano hilo, kampuni ya HUAWEI siku hiyo ya Alhamisi ilizindua rasmi awamu ya tisa ya shindano hilo la kimataifa la TEHAMA 2024-2025, mpango wa kila mwaka unaokuza ujuzi wa TEHAMA miongoni mwa wanafunzi, huku kujiandikisha mtandaoni kukifunguliwa hadi mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha