Maelfu ya watu wa China waburudika katika “Wikendi ya Supa Marathon”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2024
Maelfu ya watu wa China waburudika katika “Wikendi ya Supa Marathon”
Tarehe 3, Novemba, 2024, washiriki wa mbio za marathon za Beijing wakipita Uwanja wa Tian’anmen. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Maelfu ya watu nchini China walikimbia barabarani siku ya Jimapili, siku ambayo imesifiwa kuwa “Wikendi ya Supa Marathon” ya China.

Takwimu zimeonesha kuwa katika siku moja tu ya Jumapili, mbio zaidi ya 30 za marathon zimefanyika katika miji mbalimbali nchini China, ikiwemo pamoja na miji ya Beijing, Hangzhou na Xi'an. Mbio hizo zimevutia washiriki zaidi ya 450,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya washiriki wa mbio za marathon za China imeongezeka kwa kasi. Mnamo mwaka 2023, mashindano karibu 700 ya mbio za marathon yalikuwa yamefanyika China. Hasa katika mwanzo wa majira ya mchipuko na mwisho wa majira ya mpukutiko, shughuli za Siku ya Mbio zinafanyika katika miji mbalimbali na kuvutia wapenda mbio kushiriki shughuli hiyo yenye furaha kubwa kama kanivali.

Wang Zongping, profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Uhandisi cha Nanjing alisema, "Inayostahiki kufuatiliwa ni kuwa, mbio za marathon zimekuwa shughuli zinazopendwa zaidi na watu wengi katika miji ya China. Wimbi hili siyo tu limehusisha wanariadha wa weledi, bali pia linavutia watu wa kawaida wanaopenda kufanya shughuli za kujenga mwili.

Shughuli za mbio za marathon sasa zimekuwa msukumo muhimu wa uchumi wa China. Kila shughuli ya mbio huleta mapato ya mamilioni ya dola za Marekani kutokana na huduma za safari, hoteli na matumizi ya vifaa. Shughuli hizo pia zinasaidia kuonesha utamaduni mbalimbali wa miji na kuongeza sifa za miji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha