

Lugha Nyingine
Shandong Laixi: Uundaji wa ndege nzima waharakishwa, uchumi wa anga ya chini "waruka juu"
Novemba 3, 2024, hali ya pilikapilika ilionekana kwenye mstari wa uundaji wa ndege katika Kampuni ya Uundaji wa Ndege ya Alamasi ya Wanfeng ya Qingdao, ambapo maofisa wa Forodha ya Dagang ya Qingdao walikuwa wakisimamia kazi husika.
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Laixi wa Qingdao mkoani Shandong umetumia nguvu bora ya mazingira yake kuharakisha maendeleo ya viwanda vya uundaji wa ndege nzima, na kuingiza miradi bora ya viwanda hivyo, huku ukitekeleza miradi 12 ikiwemo uundaji wa ndege nzima za kutua, utengenezaji wa vipuri, na huduma za urukaji wa ndege. Mji huo umeendelea kupata mafanikio siku hadi siku katika uundaji wa doroni, na utoaji mafunzo ya urukaji, na oda zake nyingi zaidi zinatoka katika nchi za Amerika Kaskazini, Ulaya na maeneo mengine.
Picha na Zhang Jinggang (vip.people.com.cn)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma