Kampuni za Misri zajiandaa Maonyesho ya 7 ya CIIE ya China zikiangalia soko kubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2024
Kampuni za Misri zajiandaa Maonyesho ya 7 ya CIIE ya China zikiangalia soko kubwa
Wafanyakazi wakihamisha ketchup zinazopakiwa kwenye mstari wa uzalishaji wa Shirika la Swiss la Misri jimboni Sharqia, nchini Misri, Oktoba 27, 2024.(Xinhua/Ahmed Gomaa)

Wakati inapokaribia kufunguliwa kwa Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE), kampuni za Misri zinazoshiriki kwenye maonyesho hayo zinajiandaa, zikitarajia kupata fursa katika soko kubwa la China.

Miongoni mwa kampuni za Misri zitakazoshiriki kwenye Maonyesho ya CIIE ya mwaka huu, iliyopangwa kufanyika huko Shanghai tarehe 5 hadi tarehe 10 Novemba, ni Kampuni ya Linah Farms, wazalishaji wakuu wa tende za Medjool nchini Misri na Mashariki ya Kati.

Kampuni nyingine ya Misri inayoshiriki kwenye Maonyesho ya 7 ya CIIE ni Shirika la Swiss la Misri, ambalo linalenga kuuzia unga wa ngano nchini China, na vile vile pasta na nyanya.

Meneja mkuu wa kampuni hiyo Ahmed El-Sebaie alisema kuwa kila mwezi kampuni hiyo inazalisha takriban tani 45,000 za unga wa ngano, tani 8,000 za pasta, na tani 3,000 za ketchup.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha