Xi Jinping akagua Kikosi cha Askari Miavuli cha Jeshi la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2024
Xi Jinping akagua Kikosi cha Askari Miavuli cha Jeshi la China
Tarehe 4, Novemba, Xi Jinping akikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa kikosi cha askari miavuli. (Li Gang/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) tarehe 4 alikagua kikosi cha askari miavuli cha jeshi la China.

Wakati wa ukaguzi huo alisisitiza kuwa, kikosi cha askari miavuli kinafanya kazi muhimu maalumu kwenye mfumo wa nguvu ya jeshi na mfumo wa mapigano ya vita wa jeshi la China. Ni lazima kutekeleza matakwa ya ujenzi wa muundo mpya wa Jeshi la Anga, kuimarisha kwa pande zote mazoezi ya kijeshi na maandalizi ya vita, kuongeza uwezo wa kufanya mapigano ya kivita wa kikosi cha askari miavuli, na kufanya juhudi za kujenga kikosi hicho kuwa cha mambo ya kisasa chenye nguvu kubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha