Shirika la Ndege la Ethiopian lapokea ndege ya kwanza ya abiria A350-1000 ya Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 07, 2024
Shirika la Ndege la Ethiopian lapokea ndege ya kwanza ya abiria A350-1000 ya Afrika
Ndege ya abiria A350-1000, iliyopewa jina la "Ethiopia: Eneo la Chimbuko," ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Novemba 5, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Shirika la ndege la Ethiopian limepokea ndege ya kwanza ya abiria A350-1000 na kuwa shirika la ndege la kwanza la Afrika kutumia ndege kubwa zaidi ya aina mfululizo za ndege ya A350.

Ndege hiyo ya abiria iliyopewa jina la "Ethiopia: Eneo la Chimbuko," ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Jumanne.

Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopian, Mesfin Tasef alisema katika hafla ya kukaribisha rasmi ndege hiyo, kwamba kwa kuongezwa kwa ndege A350-1000, shirika hilo litapanua ushawishi wake duniani na kuunganisha maeneo zaidi katika mabara matano.

Katika ndege ya A350-1000 kuna viti 395 vya daraja la juu na la kawaida kwa abiria, na kuifanya kuwa ndege kubwa zaidi kati ya ndege za Shirika la ndege la Ethiopian.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha