Lugha Nyingine
Kivutio cha Potatso chenye mandhari nzuri huko Shangri-la, Mkoani Yunnan
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2024
Mandhari ya Eneo la kivutio cha Potatso huko Shangri-la ni kama picha ya kuchorwa. (Picha na Chu Chengjiang) |
Katika mwisho wa majira ya mpukutiko na mwanzo wa majira ya baridi, eneo la kivutio cha Potatso lilichoko Mji wa Shangri-la wa Eneo linalojiendesha la Kabila la Watibet la Diqing, Mkoani Yunnan kimekuwa na rangi mbalimbali, za nyekundu, njano, na bluu, na misitu, maziwa na nyasi zimeunda mandhari nzuri katika mwanzo wa majira ya baridi, na kuvutia watalii wengi kuja huko.
Eneo la kivutio cha Potatso liko umbali wa kilomita 22 kutoka Mji wa Shangri-La, lina ukubwa wa takriban kilomita za mraba 1,313. Pamoja na rasilimali nyingi kama vile maziwa na ardhi oevu, misitu na nyasi, mabonde ya mito na vijito, wanyama na mimea adimu, eneo hilo ni hifadhi muhimu ya viumbe anuai na kizuizi cha usalama wa ikolojia.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma