Lugha Nyingine
Kenya inatumai kuimarisha mawasiliano na China katika sekta za utalii na utamaduni
Gari la watalii likiendeshwa kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara nchini Kenya Oktoba 12, 2024. (Xinhua/Han Xu) |
Kenya imesisitiza dhamira yake ya kuimarisha mawasiliano kati yake na China katika sekta za utalii na utamaduni kwenye msingi wa mkutano wa kilele wa Baraza la 2024 la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika kwa mafanikio mwezi Septemba katika mji mkuu wa China Beijing.
Kaimu waziri wa utalii wa Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya Kenya, Benard Kahuthia alisisitiza uhusiano wa wenzi wa kudumu kati ya Kenya na China uliokita mizizi katika kuheshimiana na kuwa na matarajio ya pamoja ya ukuaji.
Naibu waziri wa Utalii na Utamaduni wa China, Lu Yingchuan na maofisa wa huko Narko pia walishiriki kwenye hafla husika.
Shughuli za utalii siku zote ni jiwe la msingi wa uchumi wa Kenya. Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inatafuta njia ya kuongezeka kwa idadi ya watalii wa China na kuimarisha zaidi mawasiliano ya kitamaduni na China.
"Katika miaka mingi iliyopita, China imekuwa moja ya soko la chanzo cha watalii nchini Kenya, ambayo ni mshirika wa maendeleo ya miundombinu na mawasiliano ya kitamaduni, na imechangia maendeleo ya nchi yetu," Kahuthia alisema na kuongeza kuwa, "Ushirikiano tunaopongeza leo unatupa mitazamo mipya, na kuhimiza sisi kufanya utafiti, kuthamini na kuhusisha rasilimali za kipekee za nchi yetu."
Kahuthia alisema Kenya ilipokea watalii 52,865 kutoka China mwaka 2023 na inalenga kuongeza idadi ya watalii kutoka China ili kuhimiza kuongezeka kwa faida za kiuchumi na kuimarisha uhusiano wa kitamaduni.
Lu alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika sekta za utamaduni na utalii kwa kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili. Alisema serikali ya China inatilia maanani sana mawasiliano na ushirikiano kati yake na nchi za Afrika katika sekta ya utalii, na kusisitiza nguvu kubwa na mustakabali mpana wa ushirikiano kati ya China na Kenya katika sekta ya utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma