Lugha Nyingine
Kutembelea Bandari ya Doraleh yenye uwezo mkubwa nchini Djibouti
Picha iliyopigwa tarehe 8, Novemba ikionesha Bandari ya Doraleh yenye uwezo mkubwa huko Djibouti, Mji Mkuu wa Djibouti. |
Djibouti, nchi iliyopo Pembe ya Afrika ina hali ya kipekee ya kijiografia. Nchi hii inaunganishwa na Bahari ya Mediterania na Bahari ya Hindi kwa kupita Mfereji wa Suez, Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden, upande wake wa magharibi unaelekea sehemu za ndani barani Afrika. Bandari ya Djibouti iko kwenye mazingira mazuri ya asili, na ina nguvu kubwa ya kujiendeleza. Shughuli za mawasiliano na uchukuzi , biashara na huduma, ambazo utoaji huduma ni shughuli kuu ya bandari hiyo, ambayo inachukua asilimia 80 hivi ya pato la taifa la Djibouti.
Bandari ya Doraleh yenye uwezo mkubwa, ambayo Kundi la Biashara la China limeshiriki kwenye uwekezaji na uendeshaji wake ilizinduliwa rasmi mwaka 2017. Usanifu wa uwezo wa kupakia na kupakua bidhaa wa Bandari hiyo ni tani milioni 7.08 kila mwaka, na uwezo wa kushughulikia makontena sanifu 200,000 kila mwaka, bandari hiyo imekuwa moja kati ya bandari za kisasa zaidi katika Afrika Mashariki.
(Picha na Wang Guanlin/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma