Mjumbe Maalum wa China atoa wito wa kutoa juhudi za pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2024
Mjumbe Maalum wa China atoa wito wa kutoa juhudi za pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Liu Zhenmin, mjumbe maalum wa China kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Brussels, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Liu Xuxuan)

BRUSSELS - Nchi zilizoendelea na zinazoendelea lazima zifanye kazi pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mjumbe maalum wa China kuhusu mabadiliko ya tabianchi Liu Zhenmin amesema, akibainisha kuwa China itashirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na pande nyingine ili kuendeleza utekelezaji wa Mkataba wa Paris.

Liu ametoa kauli hiyo mjini Brussels katika mahojiano yake na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni kabla ya kuondoka kuelekea Baku, Azerbaijan, kuhudhuria Mkutano wa 29 wa Nchi Watia saini kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29).

Nchi zilizoendelea zinapaswa kuongoza kutoa usaidizi wa kifedha kwa nchi zinazoendelea katika kushughulikia changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, Liu amesema, akiongeza kuwa ni wajibu wao ulioainishwa katika Mkataba wa Paris.

Kwenye mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa Mwaka 2009 mjini Copenhagen, nchi zilizoendelea ziliahidi kutoa dola bilioni 100 za Kimarekani kwa mwaka katika ufadhili wa tabianchi ili kuunga mkono nchi zinazoendelea katika kubadilisha muundo wa nishati kuwa nishati mbadala; hata hivyo, ahadi hii bado haijatimizwa kikamilifu.

"Ufadhili huu ni wa kiasi ikilinganishwa na rasilimali nyingi zinazohitajika katika kubadilisha muundo wa nishati kuwa nishati mbadala duniani, lakini umetumika kama kielelezo cha ushirikiano mzuri wa kimataifa," Liu amesema. Unaweza pia kutoa mchango mkubwa katika kutumia fedha za soko la kimataifa na kuhimiza uwekezaji wa kibinafsi, ameongeza.

Huku COP29 unatarajiwa kuweka mipango ya malengo ya ufadhili wa tabianchi duniani zaidi ya Mwaka 2025, Liu anaamini kuwa haitakuwa rahisi kwa mazungumzo husika ya kifedha kusonga mbele bila matatizo.

China, kama nchi inayoendelea, imekuwa ikitekeleza kikamilifu ahadi yake ya mageuzi ya kijani, Liu amesema.

Amesema, China inasonga mbele kwa nguvu zote katika matumizi ya umeme kwenye sekta ya mawasiliano ya usafiri, na reli za mwendo kasi zimekuwa njia kuu ya usafirishaji kwa umma huku matumizi ya magari yanayotumia umeme yakiongezeka kwa kasi, ikipunguza utoaji wa gesi chafuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha