Laini maalum ya basi yasaidia wanakijiji kuuza bidhaa za kilimo mkoani Guizhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2024
Laini maalum ya basi yasaidia wanakijiji kuuza bidhaa za kilimo mkoani Guizhou, China
Wakulima wakifanya kazi shambani katika Kijiji cha Xiaba, Wilaya ya Wudang, Mjini Guiyang, Mkoani Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Novemba 6, 2024. (Xinhua/Yang Wenbin)

Basi Na. 252, linalopita kati ya eneo la kijijini na eneo la mjini la Guiyang katika Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, lilianzisha laini maalum mwezi Juni mwaka huu kuwezesha wanavijiji kuuza mazao yao ya kilimo.

Kila siku, idadi kubwa ya wakulima huchukua laini hiyo maalum ya basi hadi mjini ili kuuza mazao yao waliyozalisha shambani. Rafu na kamba za ngozi pia zimefungwa kwenye basi hilo kusaidia kubeba vikapu vya mboga za majani vya wakulima.

Kwa kufunguliwa kwa laini hiyo maalum ya basi, muda wa matunda na mboga za majani kufika mjini umepunguzwa kutoka zaidi ya saa moja hadi dakika takriban 40, na hali ya usafiri wa wakulima pia imeboreshwa sana. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha