Mkutano wa COP29 wafunguliwa nchini Azerbaijan huku Dunia ikitafuta lengo jipya la ufadhili wa mabadiliko ya Tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2024
Mkutano wa COP29 wafunguliwa nchini Azerbaijan huku Dunia ikitafuta lengo jipya la ufadhili wa mabadiliko ya Tabianchi
Mkutano wa COP29 wafunguliwa nchini Azerbaijan huku Dunia ikitafuta lengo jipya la ufadhili wa mabadiliko ya Tabianchi

BAKU – Mkutano wa 29 wa Nchi Watia saini kwenye Mkataba wa Mfumokazi wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), au COP29, umefunguliwa katika mji mkuu wa Azerbaijan wa Baku jana Jumatatu.

Mkutano wa COP29 wa mwaka huu unalenga kutafuta lengo jipya la ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi ili kuchukua mbadala wa lengo la pamoja lililopo sasa la nchi zilizoendelea kuhamasisha na kutoa dola za kimarekani bilioni 100 kwa mwaka kuunga mkono nchi zinazoendelea.

Mkutano huo, uliopangwa kufanyika Novemba 11-22, pia utaangazia mada kama vile soko la biashara ya kaboni duniani, pamoja na kubadilisha muundo wa nishati duniani kuwa nishati mbadala kutoka kwenye nishati ya kisukukuu.

Lengo jipya "lazima liwe fanisi na toshelezi" kushughulikia matatizo ya dharura, amesema Mukhtar Babayev, rais mteule wa COP29 ambaye pia ni waziri wa ikolojia na maliasili wa Azerbaijan katika hafla ya ufunguzi.

Ameongeza kuwa lengo hilo pia linapaswa "kushughulikia mahitaji na vipaumbele vya nchi zinazoendelea" na kujumuisha vipengele vya kina vyenye ubora.

Pande husika "lazima zikubaliane juu ya lengo jipya la ufadhili wa tabianchi duniani," amesema Simon Stiell, katibu mtendaji wa UNFCCC, akitoa wito kwa washiriki kufanya kazi kwa bidii ili kuufanyia mageuzi mfumo wa mambo ya fedha duniani.

COP, au Mkutano wa Nchi Watia saini, unarejelea mfululizo wa mikutano rasmi ambapo serikali za nchi hizo kutathmini juhudi za kimataifa za kuendeleza Makubaliano ya Paris na Mkataba wa Mfumokazi wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, kwa lengo la kuweka kikomo cha ongezeko la joto duniani katika nyuzi joto 1.5.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha