Waziri Mkuu wa Visiwa vya Shelisheli akiri kushindwa katika uchaguzi wa wabunge

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2024
Waziri Mkuu wa Visiwa vya Shelisheli akiri kushindwa katika uchaguzi wa wabunge
Wafanyakazi wakihesabu kura mjini Triolet, Shelisheli, Novemba 11, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

PORT-LOUIS - Waziri Mkuu wa Visiwa vya Shelisheli Pravind Kumar Jugnauth ametangaza jana Jumatatu kukiri kushindwa kwa muungano wake wa vyama vya siasa katika uchaguzi wa wabunge, kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumapili.

"Ni wazi kwamba Muungano wa Lepep unaelekea kushindwa sana," Jugnauth amewaambia waandishi wa habari muda mfupi kabla ya saa 8 mchana, kwa saa za Shelisheli.

"Nilifanya kila nilichoweza kwa ajili ya nchi na watu. Wananchi wamechagua timu nyingine ya kuongoza nchi. Naheshimu chaguo hilo," amesema. "Naitakia nchi yangu na watu mafanikio mema."

Matokeo kamili ya uchaguzi huo yalikuwa yakitarajiwa kutangazwa jana Jumatatu. Kiongozi wa chama, au muungano vyama wenye kupata wabunge wengi, atateuliwa kuwa waziri mkuu baadaye.

Matokeo ya awali katika majimbo matano ya uchaguzi yalikuwa yakionyesha kuwa wagombea kutoka Muungano wa Mabadiliko, unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Navin Ramgoolam, walikuwa wakiongoza sana na kuelekea kupata ushindi wa wazi.

Kwa mujibu wa makadirio ya waangalizi wa uchaguzi huo, mwenendo huo unapaswa kuwa hivyohivyo katika majimbo yote 21 ya uchaguzi.

Bunge la Muundo wa Baraza Moja la Mauritius lina viti 70. Wapiga kura huchagua moja kwa moja wabunge 62 wa Bunge la Kitaifa, huku wanane waliosalia wakiteuliwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha