

Lugha Nyingine
Maonesho ya Ndege ya China yaanza Zhuhai, Kusini mwa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2024
![]() |
Ndege za kivita za China za J-20 zikifanya maonesho ya ustadi wa urukaji kwenye Maonesho ya Ndege ya China huko Zhuhai, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 12, 2024. (Xinhua/Liang Xu) |
Maonyesho ya 15 ya Kimataifa ya Ndege na Vyombo vya Anga ya Juu ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonesho ya Ndege ya China (Airshow China), yameanza Jumanne huko Zhuhai, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.
Kwenye maonesho hayo, ndege za kivita za China za J-20 na J-35A, na ndege za kivita za Russia za Su-57, zimefanya maonesho ya ustadi wa urukaji angani moja baada ya nyingine. Hiyo ni mara ya kwanza kwa aina tatu hizo za ndege za kivita kutoka China na Russia kuweza kuonekana kwa wakati mmoja kwenye Maonesho ya Ndege ya China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma