

Lugha Nyingine
Vijana wa China wauza vitabu kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni (5)
![]() |
Zhang Quan (kulia) akimpiga video Dong Lu ili kutembeza vitabu katika Kampuni ya New Buds ya Uchapishaji ya Tianjin, Kaskazini mwa China, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue) |
Dong Lu, mtangazaji wa kuuza vitabu moja kwa moja mtandaoni katika Kampuni ya New Buds ya Uchapishaji ya Kundi la Vyombo vya Habari na Uchapishaji la Tianjin, na Zhang Quan, msimamizi wa matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, wameleta vitabu vyenye sifa nzuri kwa hadhira. Katika Siku ya manunuzi ya China ya Tarehe 11, Novemba, matangazo yao ya kuuza vitabu moja kwa moja mtandaoni karibu kwa saa tatu yalivutia watazamaji zaidi ya 10,000, yakipata thamani nzuri ya mauzo ya vitabu.
"Lengo la kutangaza moja kwa moja mtandaoni ni kuongoza wazazi wa watoto katika kuchagua vitabu vizuri," Dong amesema. Dong ni mmoja kati ya vijana wanaoitwa “Kizazi Z (Gen Z)", ambacho ni watu waliokua sambamba na maendeleo ya kasi ya mtandao wa intaneti na teknolojia ya habari. Akiwa mtangazaji wa moja kwa moja mtandaoni, anaamini kuwa ingawa namna ya biashara imebadilika, nia ya awali ya kutambulisha vitabu vya kuvutia kwa wateja inaendelea kuwepo.
Hadi kufikia Desemba 2023, idadi ya jumla ya watangazaji wa matangazo ya bidhaa moja kwa moja mtandaoni imefikia milioni 15.08 nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma