

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China asisitiza wajibu sawa na majukumu tofauti katika kuimarisha usimamizi tabianchi duniani
BAKU - Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa China Jumanne wakati akihutubia Mkutano wa Viongozi wa Dunia wa Hatua za Tabianchi wa Mkutano wa 29 wa Watiasaini kwenye Mkataba wa Mfumokazi wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) mjini Baku, Azerbaijan amesema kuwa kanuni ya wajibu sawa na majukumu tofauti ni msingi wa kuimarisha usimamizi wa tabianchi duniani.
Ametoa salamu za Rais Xi kwa Azerbaijan kuwa mwenyeji wa mkutano huo, akisisitiza kuwa rais Xi wa China anathamini sana juhudi na mchango wa Azerbaijan katika kuhimiza usimamizi bora wa tabianchi duniani ikiwa rais wa zamu wa COP29, na kuutakia mkutano huo mafanikio kamili.
Akisema kuwa mwaka huu inatimia miaka 30 tangu kuanza kutekelezwa kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Ding amesema pande husika lazima zifanye kazi pamoja ili kufikia matokeo ya kuridhisha ya COP29 katika mwanzo mpya, zikikidhi matarajio makubwa ya jumuiya ya kimataifa.
Amesema kuwa nchi zilizoendelea zinapaswa kuonyesha matarajio makubwa, kuchukua uongozi katika kupunguza utoaji wa hewa chafu, na kuweka malengo ya awali ya kufikia usawazishaji wa utoaji hewa ya kaboni, huku nchi zinazoendelea zinapaswa pia kufanya juhudi zao bora ndani ya uwezo wao.
Kushughulikia mabadiliko ya tabianchi hatimaye kunahitaji mageuzi ya kimsingi katika miundo ya maendeleo, Ding amesema, akiongeza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuharakisha kubadilisha muundo wa nishati kwa namna ya haki, yenye utaratibu na usawa, kudumisha utulivu wa minyororo ya viwanda na usambazaji wa nishati mpya, kuhimiza ufikiaji na uvumbuzi katika bidhaa na teknolojia za kijani, na kuharakisha kukuza nguvukazi mpya yenye sifa bora.
“China ina nia ya kufanya kazi na pande zote, ikiongozwa na maono ya ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu, ili kulinda kwa pamoja dunia yetu ya pamoja na kujenga dunia safi na yenye kupendeza,” ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma