Siku ya Watoto Duniani: Kikosi cha madaktari wa China nchini Namibia chafanya upimaji wa afya kwa watoto wa eneo la makazi ya hali duni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2024
Siku ya Watoto Duniani: Kikosi cha madaktari wa China nchini Namibia chafanya upimaji wa afya kwa watoto wa eneo la makazi ya hali duni
Daktari wa China akifanya upimaji wa afya ya kinywa kwa watoto kwenye Kituo cha Mafunzo ya Usanii cha Frans kilichoko karibu na Windhoek, mji mkuu wa Namibia,Tarehe 20 Novemba.

Tarehe 20 Novemba ni Siku ya Watoto Duniani, madaktari wanne wa kikosi cha 16 cha madaktari wa China nchini Namibia walifika asubuhi mapema kwenye Kituo cha Mafunzo ya Usanii cha Frans, kilichoko umbali wa kilomita 20 kutoka Windhoek, mji mkuu wa Namibia, na kutoa huduma za upimaji wa mwili na kinywa kwa wanafunzi 45 wanaosoma katika kituo hicho ambao wanaishi kwenye eneo la makazi ya hali duni, na madaktari wamewaletea pia vifaa vya masomo, vya uchoraji picha na vyakula.

(Picha na Chen Cheng/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha