Treni mpya ya umeme ya SGR iliyozinduliwa nchini Tanzania yasafirisha abiria milioni 1 katika muda wa miezi minne

(CRI Online) Novemba 22, 2024
Treni mpya ya umeme ya SGR iliyozinduliwa nchini Tanzania yasafirisha abiria milioni 1 katika muda wa miezi minne
Treni ya umeme ya SGR ikisimama kwenye Kituo cha Dar es Salaam nchini Tanzania Agosti 1, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Fredy Mwanjala alisema Jumatano kuwa takriban abiria milioni 1 wamesafiri kwa treni za umeme za (SGR) kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, nchini Tanzania, tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo miezi minne iliyopita.

Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa umma Bw. Mwanjala amesema kuwa idadi hiyo ni mara mbili ya jumla ya abiria wanaotumia reli ya zamani ya MGR kati ya vituo vitatu kwa mwaka.

Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 1 alizindua rasmi shughuli za kibiashara za huduma ya treni ya SGR nchini kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Shughuli za majaribio za kibiashara za huduma ya treni hiyo zilianza Julai.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha