Lugha Nyingine
Uganda na Kampuni ya China Huawei zaanzisha Maonyesho ya Nafasi za Ajira ya kila mwaka ili kukuza ajira katika sekta ya Tehama
Mshiriki akimuonyesha mkono wa bandia kwa Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja (Kulia) kwenye Maonyesho ya Nafasi za Ajira huko Kampala, Uganda, Novemba 21, 2024. (Picha na Ronald Ssekandi/Xinhua) |
Serikali ya Uganda na Kampuni ya China Huawei zimeanzisha maonyesho ya nafasi za ajira kwa siku mbili ambayo inalenga kuhimiza ajira za vijana katika sekta ya Tehama.
Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja, ambaye aliongoza ufunguzi wa maonyesho hayo, alisema serikali imeweka kipaumbele Tehama katika mipango yake ya maendeleo kwa ajili ya uboreshaji wa kijamii na kiuchumi wa nchi hiyo.
Alisema kuwa nchini Uganda, wafanyakazi wa sekta ya Tehama ni zaidi ya milioni 1.3, na imeongezeka kwa asilimia 14.8, ambayo ni ongezeko dhahiri kuliko lile la 6% la mwaka la uchumi wa nchi hiyo kwa mwaka.
Zhang Lizhong, Balozi wa China nchini Uganda alisema kuwa sekta ya Tehama ni nguvu muhimu ya kukuza maendeleo.
Balozi huyo alisema kuwa katika miaka mingi iliyopita, China ilishirikiana na Uganda katika kukuza sekta yake ya Tehama. Chini ya Mradi Mkongo wa Miundombinu ya Kitaifa wa Uganda unaofadhiliwa na China na kujengwa na Kampuni ya Huawei, kebo za kusafirisha umeme zenye urefu wa zaidi ya maili 1,864 zimewekwa, na huduma za intaneti ya 4G zimepanua katika maeneo mbali, na kuleta uboreshaji kwa sekta nyingi zikiwemo afya, kilimo na elimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma