Wanakijiji wa Mkoa wa Xinjiang Kaskazini Magharibi mwa China waliohamishiwa makazi mapya wakumbatia maisha bora (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2024
Wanakijiji wa Mkoa wa Xinjiang Kaskazini Magharibi mwa China waliohamishiwa makazi mapya wakumbatia maisha bora
Picha hii ya droni iliyopigwa tarehe 6 Novemba 2024 ikionyesha magari yakiendeshwa kwenye eneo la zamani la kivutio cha utalii la Kijiji cha Daliyabuyi cha Wilaya ya Yutian ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Xinhua/Chen Shuo)

YUTIAN - Kijiji cha Daliyabuyi cha Wilaya ya Yutian ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China hapo zamani kilikuwa kiko katikati ya Jangwa la Taklimakan. Mwaka 2019, kijiji hicho kizima kilikamilisha uhamishwaji wake na kuhamia eneo la makazi karibu na mji wa wilaya. Kutokana na hali hiyo kijiji hicho kilimaliza historia yake ya awali ya kero za usafiri, mtandao, umeme, maji ya kunywa, matibabu na shule.

Hivi sasa kijiji hicho kimeanzisha ushirika wa kilimo na ufugaji na kuendeleza utalii maalum kama vile utalii wa jangwa na kipato cha wanakijiji kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha