Lugha Nyingine
Moto mkubwa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila wasababisha familia 2,000 kupoteza makazi
Askari wa Zimamoto wakijaribu kuzima moto mkubwa uliokuwa ukiteketeza eneo la makazi duni mjini Manila, Ufilipino, Novemba 24, 2024. (Xinhua/Rouelle Umali) |
MANILA - Familia takriban 2,000 zimepoteza makazi yao baada ya moto mkubwa kukumba jumuiya ya makazi katika mji wa Manila, mji mkuu wa Ufilipino, siku ya Jumapili, viongozi wa eneo hilo wamesema, ambapo Askari wa Zimamoto Alejandro Ramos wa Idara ya Zimamoto ya Jiji la Manila amewaambia waandishi wa habari kuwa moto huo, ambao ulizuka majira ya asubuhi katika jiji hilo, imeteketeza nyumba takriban 1,000 zilizojengwa kwa nyenzo nyepesi na zinazoweza kuwaka moto.
Jeshi la Anga la Ufilipino lilitumia helikopta kunyunyuzia maji juu ya paa za nyumba zilizokuwa zikiungua za wakazi haramu karibu na Ghuba ya Manila.
Walinzi wa Pwani wa Ufilipino pia walituma boti nne za zimamoto kusaidia kudhibiti moto huo.
Malori takriban 30 ya zimamoto yalikusanyika katika eneo la tukio ili kusaidia kudhibiti moto huo.
Hata hivyo, Ramos amesema kuwa upepo mkali uliokuwa ukivuma kutoka kwenye ghuba hiyo ulisababisha moto huo kueneza kwa kasi.
Amesema kuwa mitaa myembamba ilitatiza juhudi za kudhibiti moto huo na kwamba wakazi waliokuwa wakikimbia kujiokoa na moto huo walijaza mitaa, ikifanya kuwa vigumu kwa wazima moto kupenya eneo hilo.
Ofisi ya Kupunguza Hatari za Maafa ya Manila imetangaza kuwa moto huo umezimwa majira ya saa 8 mchana, kwa saa za Manila.
Imesema, hadi kufikia sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa, ingawa baadhi ya askari wa zimamoto walipata majeraha na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma