Jeshi la Sudan lakalia tena mji mkuu wa Jimbo la Sinnar katikati mwa Sudan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2024
Jeshi la Sudan lakalia tena mji mkuu wa Jimbo la Sinnar katikati mwa Sudan
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakishiriki maandamano ya kushangilia kukalia tena Mji wa Singa, huko Omdurman, Sudan, Novemba 23, 2024. (Picha na Osman Al-Jundi/Xinhua)

PORT SUDAN - Serikali ya Sudan imetangaza siku ya Jumamosi kuwa Jeshi la Sudan (SAF) limefanikiwa kurudisha tena Mji wa Singa, mji mkuu wa Jimbo la Sinnar katikati mwa Sudan, ambao ulikuwa unadhibitiwa na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF).

"Leo (Jumamosi), Mji wa Singa umerejea kwa nchi ... Wakati wa haki utafika na kuwajibisha wale wote wanaohusika na uhalifu huu. Wahalifu watawajibishwa kwa matendo yao," Khalid Aleisir, waziri wa utamaduni na habari wa Sudan amesema katika taarifa.

Amesema, " bila kujali matishio ya ndani ya nje yatakuwa ya namna gani, watu wa Sudan watashikilia imani yao thabiti isiyoyumba kwa vikosi vyao vya kijeshi, vikosi vya upelelezi na vikosi vingine vya kawaida, vikosi vya pamoja na vikosi vilivyohamasishwa.

RSF imekuwa ikiudhibiti mji huo wa Singa kwa miezi kadhaa. Tokea mwanzo wa mwezi Oktoba, SAF imekuwa ikipigana na RSF katika eneo hilo ili kufukuza vikosi hivyo vya wanamgambo nje ya jimbo hilo.

SAF imefanikiwa kurudisha tena miji muhimu katika jimbo hilo kutoka kwa RSF, ikiwa pamoja na miji ya Al-Dinder, Al-Suki, na eneo la kimkakati la Jebel Moya, njia panda inayounganisha majimbo ya Gezira, White Nile na Sinnar.

Sudan imesumbuliwa siku zote katika mgogoro mbaya kati ya SAF na RSF tokea katikati ya Aprili Mwaka 2023. Kwa mujibu wa taarifa mpya zaidi na Mradi wa Takwimu za Eneo na Matukio ya Migogoro ya Kivita, mgogoro huo mbaya umesababisha vifo vya watu zaidi ya 27,000.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha