

Lugha Nyingine
Msichana wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 24 apata ujuzi wa ufundi mjini Tianjin, China (2)
Katika Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Mwaka 2024 uliofanyika hivi karibuni mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Kalkidan, msichana wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akitoa maelezo kwa washiriki wa mkutano huo kuhusu jukwaa la mafunzo ya mambo ya roboti za viwandani kwenye banda la Karakana ya Luban ya Ethiopia.
Kalkidan alikuwa akipata mafunzo hadi Septemba ya mwaka huu katika Karakana hiyo ya Luban nchini Ethiopia tangu Mwaka 2021. Ikiwa ilianzishwa na Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu cha Tianjin (TUTE) na Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi ya Serikali ya Ethiopia, karakana hiyo inashughulikia utengenezaji wa roboti zinazotumika viwandani, mechatroniki, udhibiti wa kiviwanda, na teknolojia ya vihisi vya viwandani, ikitoa ujuzi muhimu kwa wanafunzi wa Ethiopia katika nyanja mbalimbali za teknolojia.
Kwa sasa, Kalkidan anasoma uhandisi wa habari na mawasiliano ya simu katika TUTE. "Nimefurahishwa sana na mtindo wa elimu ya ufundi hapa, ambao unazingatia kuunganisha kwa karibu elimu ya ufundi stadi na mahitaji ya kiviwanda," amesema, akiongeza kuwa atarejea katika nchi yake baada ya kuhitimu ili kusaidia kuendeleza watu wengi zaidi wenye ufundi na ufundi stadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma