Hali ya maisha ya panda wazaliwa wa ng’ambo baada ya kurejea China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2024
Hali ya maisha ya panda wazaliwa wa ng’ambo baada ya kurejea China
Panda Xiang Xiang akila machipukizi ya mianzi katika Makazi ya Panda ya Bifengxia ya Kituo cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda wa China cha Mji wa Ya'an, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Juni 12, 2024. Xiang Xiang, panda jike, alizaliwa katika Bustani ya Wanyama ya Ueno huko Tokyo, Japan Juni 12, 2017. (Xinhua/Xu Bingjie)

Panda ni wanyama wazaliwa wa China peke yake ambao wanapendwa kote duniani, Panda wamekuwa wakipelekwa katika nchi mbalimbali duniani wakiwa kama mabalozi wa urafiki wanaoonesha nia njema ya watu wa China. Tokea miaka ya 1990, China imekuwa ikifanya juhudi za utafiti wa pamoja wa ulinzi wa Panda na taasisi 26 za nchi 20 duniani.

Kwa ujumla, watoto wa panda wanaozaliwa ng'ambo hurudishwa China wanapofikia umri fulani. Panda walirejeshwa kutoka ng'ambo, wengi wao wanaishi katika Kituo cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda wa China au Kituo cha Utafiti wa Kuzaliana kwa Panda cha Chengdu. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha