Yangzhou, Jiangsu, China: Boriti ya Daraja la Tongtaiyang la Reli ya Mwendokasi ya Beiyanjiang yaunganishwa kwa mafanikio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2024
Yangzhou, Jiangsu, China: Boriti ya Daraja la Tongtaiyang la Reli ya Mwendokasi ya Beiyanjiang yaunganishwa kwa mafanikio
Picha hii iliyopigwa Novemba 25 ikionyesha eneo la ujenzi wa boriti inayovuka Barabara Kuu ya Shanghai-Shaanxi ya Daraja la Tongtaiyang la Reli ya Mwendokasi ya Beiyanjiang, nchini China. (Picha kutoka vip.people.com)

Boriti ya urefu wa mita 100 inayovuka Barabara Kuu Shanghai-Shaanxi nchini China ya Daraja la Tongtaiyang la Reli ya Mwendokasi ya Beiyanjiang, inayojengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi wa Madaraja ya Shirika la Reli la China (CRCC), imeunganishwa kwa mafanikio jana Jumatatu, Novemba 25, 2024, ikiweka msingi imara kwa hatua za baadaye za kuweka boriti na utandazaji wa reli.

Daraja hilo la Tongtaiyang linapita katika miji mitatu ya Nantong, Taizhou, na Yangzhou, na ni sehemu muhimu ya mradi wa udhibiti wa sehemu ya Shanghai-Nanjing ya Reli ya Mwendokasi ya Shanghai-Chongqing-Chengdu. Reli hiyo ya Shanghai-Chongqing-Chengdu ni mojawapo ya mtandao wa kitaifa uti wa mgongo wa reli ya mwendokasi wa“Reli Nane za Wima na Nane za Mlalo,”wenye urefu wa kilomita takriban 2,100.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha