Taasisi ya Confucius nchini Uganda yaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2024
Taasisi ya Confucius nchini Uganda yaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake
Afisa elimu wa Uganda Ismail Mulindwa akitoa hotuba kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala, Uganda, Novemba 25, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

KAMPALA - Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Makerere, imefanya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake siku ya Jumatatu, ikiashiria muongo mmoja wa kuendeleza na kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni na lugha kati ya China na Uganda.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika chuo kikuu hicho, ilishirikisha maonyesho ya kitamaduni kama vile nyimbo na ngoma za China. Wajumbe kutoka China, wahadhiri na walimu wa chuo kikuu hicho, na wawakilishi wa jumuiya ya Wachina wanaoishi Uganda walishiriki kwenye hafla hiyo.

Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia Elimu ya Juu, John Muyingo amesifu mchango wa taasisi hiyo katika kuimarisha uhusiano kati ya Uganda na China kupitia mawasiliano ya lugha na ya kitamaduni katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, katika ujumbe wake uliotolewa na afisa elimu Ismail Mulindwa.

Muyingo amesisitiza mchango muhimu wa taasisi hiyo katika kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kichina katika shule za sekondari za Uganda na kuunga mkono ujumuishwaji wake katika masomo ya elimu ya juu.

"Nawaomba wadau wote kuendelea kuendeleza maelewano ya kitamaduni ya kuvuka mipaka, uvumbuzi na ushirikiano kwa kuwa tunapotazama mustakabali wa baadaye, kuimarisha uhusiano kati ya Uganda na China, kutumia kikamilifu nguvu za kimageuzi za upanuzi wa elimu na utamaduni kutaboresha nchi yetu," amesema waziri huyo.

Fan Xuecheng, konsuli katika Ubalozi wa China nchini Uganda, amepongeza walimu, watu wa kujitolea na wanafunzi wa taasisi hiyo kwa dhamira yao, jambo ambalo limezidisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.

"Ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Uganda unaweka mfano mzuri kwa nchi zinazoendelea kutafuta maendeleo kupitia umoja na ushirikiano. Mawasiliano ya kitamaduni na kufunzana vimekuwa sehemu muhimu na umaalum wa wazi wa ushirikiano kati ya China na Uganda," Fan amesema.

Shughuli hiyo pia imeshuhudia uzinduzi wa jumuiya mbili mpya, ambazo ni Jumuiya ya Wahitimu wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Makerere na Jumuiya ya Walimu wa Lugha ya Kichina nchini Uganda.

Maadhimisho hayo pia yameenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Confucius duniani, ikionyesha mchango wake mpana katika kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni na kielimu duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha