Mikoa ya Kaskazini mwa China yakumbwa na wimbi la baridi, dhoruba za theluji (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2024
Mikoa ya Kaskazini mwa China yakumbwa na wimbi la baridi, dhoruba za theluji
Wafanyakazi wa usafi wa mazingira wakiondoa theluji mjini Zhangjiakou, Mkoani Hebei, kaskazini mwa China, Novemba 25, 2024. (Picha na Wu Diansen/Xinhua)

HARBIN/HOHHOT - Kuanzia Jumanne, maeneo mengi katika mikoa ya Jilin na Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China yamekuwa yakishuhudia kushuka kwa joto kwa nyuzi joto zaidi ya 10.

Katika Mji wa Hegang mkoani Heilongjiang, theluji iliyoanguka kuanzia saa 2 asubuhi Jumanne hadi saa 2 asubuhi jana Jumatano imefikia 49.7 mm, ikivunja rekodi ya kihistoria ya kuanguka kwa theluji ya siku moja katika mwezi wa Novemba. Kina cha juu cha theluji cha mji huo kilikuwa kimefikia sentimita 48.

Wakati huo huo, ukiwa na kina cha theluji cha sentimita 45, Mji wa Heihe umevunja rekodi yake tangu uchunguzi wake wa hali ya hewa ulipoanza mwaka 1959.

Ingawa hali ya theluji katika maeneo mengi ya Heilongjiang imekuwa ikipungua hatua kwa hatua, ongezeko la theluji linakadiriwa kuendelea leo Alhamisi. Aidha, halijoto katika mkoa mzima inakadiriwa kushuka.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya China imeshauri wananchi kuchukua tahadhari hitajika dhidi ya wimbi la baridi, kuwa waangalifu katika kuzuia magonjwa ya kupumua na ya moyo na mishipa, na kutilia maanani usalama wanapokuwa nje.

Tangu mwanzoni mwa wiki hii, mkoa mzima wa Mongolia ya Ndani kaskazini mwa China pia umekuwa ukiathiriwa na wimbi la baridi, huku joto likishuka.

Kiwango cha chini cha halijoto katika maeneo mengi ya sehemu za kati na mashariki mwa mkoa huo kilikuwa kimepungua hadi nyuzi joto karibu 13. Katika baadhi ya maeneo, halijoto imeshuka hadi chini ya nyuzi joto 18.

Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa kuanzia Jumatano hadi Alhamisi, theluji au hata kimbunga kikubwa cha theluji kitapiga sehemu ya kaskazini-mashariki ya Mongolia ya Ndani, kikisababisha kushuka kwa joto kwa nyuzi joto 4 hadi 6.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha