Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya mnyororo wa usambazaji wa Bidhaa ya China yaonyesha utengenezaji bidhaa wa teknolojia ya hali ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2024
Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya mnyororo wa usambazaji wa Bidhaa ya China yaonyesha utengenezaji bidhaa wa teknolojia ya hali ya juu
Watu wakifahamishwa kuhusu suluhu jumuishi ya vipuri vya aluminiamu nyepesi kwenye banda la Kundi la Kampuni za CITIC katika eneo la Maonyesho ya Mnyororo wa Utengenezaji Bidhaa kwa Teknolojia ya Hali ya Juu la Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa usambazaji wa Bidhaa ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 27, 2024. (Xinhua/Zhang Chenlin)

EIJING – Yakiwa na kaulimbiu ya "Kuunganisha Dunia kwa Mustakabali wa Pamoja," Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa usambazaji wa Bidhaa ya China, yaliyoandaliwa na Baraza la China la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa, yameanza siku ya Jumanne mjini Beijing.

Maonyesho hayo ya Mwaka 2024 yameanzisha eneo jipya la maonyesho mahsusi kwa ajili ya utengenezaji bidhaa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu, likiongezwa kwenye idadi ya maeneo ya maonyesho ya mwaka jana ya nishati safi, magari ya teknolojia ya kisasa, teknolojia ya kidijitali, maisha ya afya, kilimo cha kijani na sehemu za huduma za usambazaji wa bidhaa.

Mnyororo kamili wa utengenezaji bidhaa kwa teknolojia ya hali ya juu kimataifa unaonyeshwa katika eneo hilo jipya, likijikita katika mambo manne - Utafiti na uundaji bidhaa, utumiaji wa nyenzo mpya, vipuri muhimu na usindikaji, na utengenezaji bidhaa kwa kutumia akili mnemba na vifaa vya kisasa.

Kupitia maonyesho ya bidhaa na uzoefu wa mawasiliano, wageni wanaweza kuelewa vyema mafanikio makubwa ya teknolojia mpya na matumizi ya teknolojia za kidijitali, mtandao na za akili mnemba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha