Lugha Nyingine
Waandishi wa habari wa China na wa kigeni wajionea hali ya mvuto wa soko la usiku mjini Shenzhen
Picha ya muonekano wa angani wa Bandari ya Yantian iliyopigwa kutoka Soko la Usiku la Yan'gang mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (People's Daily Online/Zhang Lulu) |
Shenzhen, mji wa pwani wenye ustawi ulioko Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, umepiga hatua kubwa katika kuendeleza uchumi wake wa usiku katika miaka ya hivi karibuni, huku Soko la Usiku la Yan'gang likiibuka kuwa kivutio kikuu.
Soko hilo hupata hali ya uhai wakati usiku unapoingia. Kitovu hiki chenye shughuli nyingi za biashara kimekuwa kivutio kwa vijana, kikitoa vitafunio vya aina mbalimbali vinavyovutia ladha za watalii.
Soko hilo la usiku hutoa hali jumuishi ya burudani mbalimbali ambayo huchanganya vyakula vitamu, maonyesho ya kitamaduni na shughuli za burudani. Mara kwa mara huwa na shughuli zenye maudhui maalum, zikiwemo za matamasha ya kimataifa ya chakula na wiki ya mambo ya kitamaduni, zikivutia watalii wa China na wa kigeni pia.
Taihe, Jiangxi, China: Ujenzi wa Daraja la Chengjiang waendelea kwa kasi
Mawimbi ya Baridi Kali Yaikumba China, Maeneo Mengi Yashuhudia Kuanguka kwa Theluji
Theluji yaanguka kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye Milima Emei, China
Mkutano wa 19 wa Viongozi wa Kundi la 20 (G20) kufanyika Rio de Janeiro
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma