Shughuli ya Kumbukumbu ya kila mwaka ya familia za wahanga wa mauaji ya halaiki ya Nanjing yafanyika (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2024
Shughuli ya Kumbukumbu ya kila mwaka ya familia za wahanga wa mauaji ya halaiki ya Nanjing yafanyika
Manusura wa Mauaji ya Halaiki ya Nanjing, Ai Yiying, Liu Minsheng, Xia Shuqin (kutoka kushoto kwenda kulia, mbele) wakishiriki kwenye shughuli ya kumbukumbu ya familia za wahanga wa Mauaji ya Halaiki ya Nanjing Desemba 1, 2024. (Xinhua/Li Bo)

NANJING – Shughuli ya Kumbukumbu ya Mwaka 2024 ya familia za wahanga wa Mauaji ya Halaiki ya Nanjing imefanywa kuanzia jana Jumapili huko Nanjing, mji mkuu wa Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China ambapo imefanyika wiki mbili kabla ya siku ya kumbukumbu ya kitaifa ya China Desemba 13, shughuli hiyo ilianzishwa rasmi miaka kumi iliyopita.

Familia za wahanga zilitoa heshima kwa wapendwa wao mbele ya "ukuta wa kilio cha yowe" nje ya Jumba la Kumbukumbu ya Wahanga katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing yaliyofanywa na Wavamizi wa Japan. Kwenye Ukuta huo yamechongwa majina ya wahanga 10,665 waliouawa katika miaka 87 iliyopita.

Mnamo Desemba 13, 1937, jeshi la wavamizi wa Japan lilikalia Nanjing, mji mkuu wa China wa wakati huo. Kwa muda wa wiki sita, wavamizi hao waliua raia na askari wasio na silaha wa China zaidi ya 300,000.

Miongoni mwa waombolezaji walioshiriki kwenye shughuli hiyo ni Xia Shuqin mwenye umri wa miaka 95. "Nitakuja ilimradi tu afya yangu inaruhusu. Ni vigumu kutokuwa hapa," amesema.

Mnamo Desemba 13, 1937, Xia aliyekuwa na umri wa miaka minane wakati huo aliponea chupuchupu katika mauaji ya kikatili, huku watu saba kati ya tisa wa familia yake ya karibu wakiwa waliuawa. Baba yake alipiga magoti na kuwasihi wasiwadhuru raia, lakini aliuawa kwa kupigwa risasi.

Mama na dada yake aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja, waliokuwa wamejificha chini ya meza, walitolewa nje na wavamizi. Walimwangusha mtoto huyo mchanga chini na kumchoma kisu hadi kufa. Baadaye, askari hao wa Japan walimbaka mama yake na kumuua.

Babu na bibi wa Xia pia waliuawa na wavamizi hao, huku dada zake wawili wakubwa walibakwa na kuuawa. Alijificha kwenye branketi na kupoteza fahamu baada ya kuchomwa kisu mara tatu.

Xia ni miongoni mwa manusura 32 walioandikishwa kwenye kumbukumbu katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing -- wakiwa na wastani wa umri wa miaka zaidi ya 94.

Serikali ya China imehifadhi ushuhuda wa manusura hao katika nyaraka za maandishi na picha za video. Rekodi hizo za mauaji ziliorodheshwa na UNESCO kwenye Kumbukumbu ya Rejesta ya Dunia Mwaka 2015.

Hata hivyo, kadiri manusura hao wanavyozidi kuzeeka na kufariki dunia, vizazi vyao vinatambuliwa kuwa muhimu kwa kupitisha kumbukumbu na kueleza ukweli kuhusu ukatili huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha