

Lugha Nyingine
Mwonekano wa Bwawa la Danjiangkou, mwanzo wa njia ya kati ya Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini wa China (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2024
![]() |
Picha iliyopigwa tarehe 30 Novemba 2024 ikionyesha mandhari ya Bwawa la Hifadhi ya Maji la Danjiangkou katika Mkoa wa Hubei, katikati mwa China. (Xinhua/Hu Jingwen) |
Mradi wa China wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini una njia tatu. Njia ya kati, ambayo ndiyo maarufu zaidi, inaanzia kwenye Bwawa la Hifadhi ya Maji la Danjiangkou Mkoa wa Hubei, katikati mwa China na inapitia mikoa ya Henan na Hebei kabla ya kufika Beijing na Tianjin.
Kikiwa ni chanzo muhimu, sifa ya maji ya Bwawa hilo la Hifadhi ya Maji la Danjiangkou imedumu juu ya kigezo cha daraja la II kwa miaka mingi.
Njia ya kati ya mradi huo ilianza kutoa maji Desemba 12, 2014. Katika miaka kumi iliyopita, njia hiyo imepeleka maji ya mita za ujazo zaidi ya bilioni 68, na imenufaisha watu zaidi ya milioni 100 katika Mkoa wa Henan wa katikati mwa China, Hebei kaskazini mwa China, Mji wa Tianjin wa kaskazini mwa China na mji mkuu, Beijing.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma