

Lugha Nyingine
Maonyesho ya sanaa ya Kazi za mikono za China yafanyika kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini (3)
![]() |
Mtu akitazama vitu vinavyooneshwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Sanaa ya Kazi za Mikono ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika Jumba la Sanaa la Chuo Kikuu cha Johannesburg mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Novemba 29, 2024. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua) |
JOHANNESBURG - Kituo cha kwanza cha Maonyesho ya Kimataifa ya Sanaa ya kazi za Mikono ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Shanghai nchini China na Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) nchini Afrika Kusini, yenye kaulimbiu ya "Mazungumzo na Tamaduni za Dunia," kimefunguliwa Afrika Kusini siku ya Ijumaa.
Shughuli hiyo ya mara ya kwanza nchini humo itafanyika kwenye Jumba la Sanaa la UJ hadi Januari 25, 2025, na kisha itaelekea hadi maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na Kazakhstan, Sweden, Uturuki, New Zealand, Australia, Ufaransa na Italia, miongoni mwa mengine.
Katika hafla ya ufunguzi, Konsela mkuu wa Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini Li Zhigang amesema maonyesho hayo yatasaidia kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni na maelewano kati ya pande mbili.
"Urithi wa utamaduni usioshikika ni hazina ya ustaarabu wa binadamu, utajiri mkubwa uliokusanywa kutoka kwa tamaduni mbalimbali katika muda mrefu. Tangu zama za kale, uchoraji na kazi za mikono zimekuwa njia ya kawaida ya mawasiliano kati ya watu duniani kote," Li amesema. "Tunatazamia mawasiliano na ushirikiano zaidi wa kitamaduni na kisanii kati ya China na Afrika Kusini katika siku zijazo."
Federico Freschi, mtendaji mkuu wa Kitivo cha Sanaa, Mitindo na Usanifu Majengo katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, amesema "Kazi za mikono si vitu tu bali ni hazina za kitamaduni zinazojumuisha historia, mila na ubunifu."
Maonyesho hayo yanaonyesha ustadi mwingi wa urithi wa utamaduni usioshikika wa China, ukionyeshwa na warithi mbalimbali. Yakiwa yamegawanywa katika sehemu tatu - Maua ya Baharini, Mtegemeano wa Vitu Vyote na Ustawi Usio na Kikomo – yanajumuisha vitu mbalimbali vya utamaduni wa jadi vya China, ikiwa ni pamoja na udarizi, ukataji karatasi, kesi ujuzi wa kufuma hariri), tiara, nianhua (michoro ya Mwaka Mpya), vyungu vya madini ya fedha na vyungu vya chai vya udongo wa zambarau, pamoja na miradi ya urithi wa utamaduni usioshikika wa aina mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma