Banda la China lafunguliwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya kuenea kwa jangwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2024
Banda la China lafunguliwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya kuenea kwa jangwa
Naibu Katibu Mtendaji wa UNCCD Andrea Meza Murillo akizungumza kwenye ufunguzi wa Banda la China kwenye Mkutano wa 16 wa Nchi Watia saini (COP16) kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Hali ya Kuenea kwa Jangwa (UNCCD) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Desemba 2, 2024. (Xinhua/Wang Dongzhen)

RIYADH - Banda la China katika Mkutano wa 16 wa Nchi Watia saini (COP16) kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Hali ya Kuenea kwa Jangwa (UNCCD) limefunguliwa rasmi Jumatatu, likiangazia juhudi na mafanikio ya China katika kukabiliana na hali ya kuenea kwa jangwa miongo kadhaa iliyopita.

Likichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 600, banda hilo la China ni la pili kwa ukubwa katika mkutano huo. Maonyesho yake, yenye kaulimbiu ya "Ukuta Mkuu wa Kijani wa Karne, Hatua ya China ya kuepusha ardhi kutoka hali ya kuenea kwa jangwa," yanaonyesha China kupambana na hali ya kuenea kwa jangwa, haswa kupitia Mpango wa Msitu wa Mikoa Mitatu ya Kaskazini, ambao ni juhudi kubwa ya kitaifa inayolenga kubadilisha hali ya kuenea kwa jangwa.

Kwenye hafla ya ufunguzi, Naibu Katibu Mtendaji wa UNCCD Andrea Meza Murillo amesifu mchango mkubwa wa China katika kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa duniani. "Nimevutiwa na picha za vizazi mbalimbali vya watu wa China wakipambana na hali ya kuenea kwa jangwa na uongozi wa China katika mchakato huu," amesema.

Guan Zhi'ou, kiongozi wa ujumbe wa China na mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Misitu na Mbuga ya China, amesema, "Katika miaka 30 tangu ijiunge na mkataba huo, China imekuwa ikitimiza wajibu wake kwa bidii, ikishiriki kikamilifu katika kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa duniani pamoja na nchi zilizopo kwenye Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja."

"China itaendelea kunufaika pamoja na teknolojia na uzoefu wake, ikitoa mchango wa busara yake na nguvu zake katika kufikia lengo la mwaka 2030 la kufikia usawazishaji wa uharibifu wa ardhi na kuendeleza mpango wa ardhi wa G20," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha