

Lugha Nyingine
Jumba jipya la Bunge la Cameroon lasimama kama ushahidi wa urafiki kati ya China na Cameroon wa kunufaishana
![]() |
Picha iliyopigwa Novemba 19, 2024 ikionyesha jumba jipya la Bunge la Taifa la Cameroon, mjini Yaounde, Cameroon. (Xinhua/Kepseu) |
YAOUNDE – Mjini Yaounde, mji mkuu wa Cameroon, jengo jipya la bunge linaonekana liking'aa sana kwenye mwanga wa jua, ambapo siku ya Jumapili, China imekabidhi funguo za jengo hilo kwa Spika wa Bunge la Cameroon Cavaye Yeguie Djibril.
"Tayari nimesikia kwamba jengo hili ni kubwa zaidi, lenye kuvutia zaidi na lenye hali nzuri isiyo na kifani katika bara nzima la Afrika," Cavaye amesema katika hotuba yake kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Kwa macho yake, jengo hilo ni zawadi ya thamani zaidi ambayo China imetoa kwa watu wa Cameroon.
"Siku hii itakumbukwa daima, ni ya kihistoria. Huu ni mfano mzuri wa urafiki wa kweli. Kama msemo unavyosema, rafiki akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli. Watu wote wa Cameroon kwa pamoja wanasema asante (kwa China)," Cavaye amesema.
Jengo hilo jipya lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu litawezesha wabunge kutekeleza kikamilifu majukumu yao ya kutunga sheria na kumaliza changamoto ya msongamano katika jengo la sasa la bunge la mabaraza mawili, amesema.
"Kwa hivyo jengo hili jipya la Bunge la Taifa linaimarisha urafiki ambao wenyewe tayari ni imara sana. Uhusiano huu mzuri umekuwa hivi kwamba, hata majanga yaliyofululiza ambayo yametikisa Cameroon katika miongo ya hivi karibuni, hayajaweza kutikisa msingi wa urafiki huu" Cavaye amesema.
Mwaka 2017, jengo la Bunge la Cameroon liliteketezwa kwa sehemu na moto. "Tukio hilo linakwama kazi ndani ya jengo hilo na ilibidi tuhamie mahali pasipofaa," Abba Alim, Mbunge wa Bunge la Cameroon, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Miaka miwili baadaye, Cavaye aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo jipya la bunge kwa ufadhili wa China. Kundi la Kampuni za Ujenzi wa Mjini la Beijing (BUCG) lilianza ujenzi huo na kazi zimekamilika ndani ya miaka mitano.
Jengo hilo jipya linajumuisha michoro ya kijadi ya mapambo ya Cameroon, huku pia likionyesha ufundi mzuri wa usanifu majengo wa China.
Cui Jinping, meneja wa mradi wa BUCG wa ujenzi wa jengo hilo jipya la Bunge, amesema, ujuzi umehamishwa na watu wa Cameroon zaidi ya 1,000 waliajiriwa wakati wa ujenzi wa mradi huo. "Wafanyakazi wa China na wafanyakazi wa Cameroon walishirikiana kukamilisha kazi za ujenzi wa mradi huu pamoja."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma