Lugha Nyingine
Huduma ya treni ya mizigo ya China-Ulaya yafikia rekodi ya kihistoria wakati treni ya safari ya 100,000 ikiwasili Ujerumani
Picha hii iliyopigwa Desemba 3, 2024 ikionyesha treni ya 100,000 ya mizigo ya China-Ulaya katika Stesheni ya Mwisho ya Kimataifa ya Duisburg (DIT), nchini Ujerumani. (Xinhua/Du Zheyu) |
DUISBURG, Ujerumani - Treni ya mizigo ya China-Ulaya ya No. X8083 ambayo ni safari ya 100,000 imewasili Duisburg, Ujerumani jana Jumanne asubuhi, ikionyesha hatua muhimu ya kihistoria kwa reli hiyo ambapo treni hiyo ambayo imetokea Chongqing, China, iliwasili kwenye Stesheni ya Duisburg saa 3: 10 asubuhi (kwa saa za Ujerumani), ikiwa imebeba vifaa vya kielektroniki, sehemu za mashine za viwandani, na vifaa vya nyumbani.
Mizigo kwenye treni hiyo imepakuliwa haraka ili kusambazwa katika maeneo mbalimbali barani Ulaya.
Mji wa Duisburg, ambao hapo awali ulijulikana kwa viwanda vyake ya chuma, sasa ni lango maarufu la biashara kati ya Ulaya na Asia. Treni za mizigo, ambazo mara nyingi hujulikana kama "ngamia wa chuma," ni sehemu muhimu ya mageuzi hayo. Treni hizo zinabeba bidhaa mbalimbali za Ulaya zinaporudi.
"Huduma hii imeongeza ufanisi wa uchukuzi na uhusiano wa kibiashara, ikionyesha mchango wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja katika kuhimiza muunganisho wa miundombinu," amesema Chang Haitao, kaimu kansela mkuu wa ubalozi wa China mjini Dusseldorf, katika hafla iliyofanyika kwenye stesheni hiyo ya Duisburg.
Kwa kutupia macho siku za baadaye, Chang amesisitiza uwezekano wa huduma hiyo kuhimiza zaidi ushirikiano na maendeleo. "Treni ya mizigo ya China-Ulaya itaendelea kuwa kichocheo cha kufungua mlango na ushirikiano, ikisukuma mbele muunganisho imara kote Eurasia na kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi duniani," amebainisha.
Markus Bangen, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Duisburger Hafen AG (Duisport), kampuni ya Ujerumani inayoendesha bandari ya Duisburg, amesema huduma hiyo ya reli inaimarisha uhusiano kati ya Ulaya na China, ikifungua soko jipya la kimataifa la usafiri ambalo linanufaisha uchumi wa nchi zote mbili.
“Duisburg inakua kwa kasi kuwa kituo kikuu katika njia ya reli hiyo, ikivutia uwekezaji, kutoa fursa za ajira na kuhimiza ukuaji katika sekta ya usambazaji” ameongeza.
Tangu mwaka 2016, safari za treni hizo kwa mwaka umeongezeka kutoka 1,702 hadi zaidi ya 17,000, huku muda wa usafiri ukiimarika, amesema Tian Zhongyu, meneja mkuu wa Kampuni ya Reli ya Kusafirisha Kontena ya China, tawi la Ulaya, akibainisha kuwa muda unaohitajika kukamilisha safari 10,000 za treni pia umepungua kutoka miezi 90 hadi miezi sita tu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma