Picha: Shuibei, "Mji Mkuu wa Vito wa China"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2024
Picha: Shuibei,

Shuibei, awali ilikuwa jina la kijiji katika Eneo la Luohu, Mji wa Shenzhen wa China. Kutokana na kukua hatua kwa hatua kwa biashara za uchakataji na uuzaji wa jumla wa dhahabu na vito, Shui Bei imekuwa nembo nzuri ya tasnia ya dhahabu na vito ya Luohu.

Baada ya miaka zaidi ya 40 ya maendeleo, tasnia ya dhahabu na vito ya Shuibei, “Mji Mkuu wa Vito wa China” imeunda mnyororo wa viwanda unaojumuisha ubunifu na utafiti, uzalishaji na utengenezaji, maonyesho na biashara, uendeshaji wa chapa, pamoja na huduma za ukaguzi na upimaji.

Hadi kufikia mwisho wa 2023, kulikuwa na karibu mashirika 20,000 ya tasnia ya vito katika Eneo la Luohu, yakiwa na mapato ya mwaka ya kibiashara ya zaidi ya Yuan bilioni 120.

Kwa sasa, serikali ya Luohu inahimiza kwa nguvu kubwa mageuzi ya Kituo cha Mkusanyiko wa Mashirika ya Dhahabu na Vito cha Shuibei kutoka kwenye uchakataji na utengenezaji wa kijadi hadi kuwa kituo cha tasnia ya hali ya juu ya kisasa, na kuwa “Mji Mkuu wa Vito wa Dunia”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha