China yagundua visukuku muhimu vya hatua za mabadiliko ya binadamu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2024
China yagundua visukuku muhimu vya hatua za mabadiliko ya binadamu
Mtaalamu wa kimataifa anayehudhuria mkutano wa kitaaluma wa eneo la Hualongdong akitembelea ukumbi wa maonyesho wa eneo la Hualongdong katika Wilaya ya Dongzhi ya Mji wa Chizhou, Mkoani Anhui, Mashariki mwa China, Desemba 6, 2024. (Xinhua/Zhou Mu)

HEFEI - Wanasayansi wa China wamegundua makumi ya visukuku vya binadamu yenye historia ya miaka 300,000, ambavyo ni ya mapema zaidi kupatikana katika Asia Mashariki kwa kujikita katika hatua za mabadiliko ya binadamu Homo sapiens, spishi ambayo binadamu wote wa sasa wanatokea.

Visukuku hivi vya binadamu, pamoja na idadi kubwa ya mifupa ya wanyama na zana za mawe, yamefukuliwa kwenye eneo la Hualongdong katika Wilaya ya Dongzhi, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China.

Watafiti wa China wametoa ripoti ya uvumbuzi na utafiti mpya zaidi kuhusu eneo hilo la binadamu ya kale la Hualongdong kwenye mkutano wa kitaaluma uliofanyika katika Wilaya ya Dongzhi kuanzia Ijumaa hadi jana Jumapili, Desemba 8. Watafiti na wasomi takriban 100, wakiwemo wataalam kadhaa wa kimataifa, wamehudhuria mkutano huo.

Likiwa liligunduliwa mwishoni mwa 1988, eneo la Hualongdong limepata matokeo makubwa kwenye ufukuaji ambao umekuwa ukiendelea tangu Mwaka 2013. Visukuku takriban 20 vya kale vya binadamu, ikiwa ni pamoja na fuvu kamili, zana za mawe zaidi ya 400, vipande vingi vya mifupa vilivyo na ushahidi wa kukatwa vipande vikubwa na vidogo, na visukuku 80 vya wanyama wenye uti wa mgongo yamechimbuliwa kwenye eneo hilo.

Kuanzia Aprili hadi Novemba 2024, timu ya kiakiolojia ilifanya raundi mpya ya ufukuaji kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 40. Jumla ya visukuku 11 vya binadamu vimegunduliwa, ikiwemo mfupa mmoja wa metatarsal wa mguu uliohifadhiwa vizuri, mfupa mmoja wa mbele uliovunjika, kipande kimoja cha katikati cha mfupa wa paja na vipande vinane vya fuvu.

Wu Xiujie, mtafiti katika Taasisi ya Masomo ya Wanyama wa Kale wenye Uti wa Mgongo and Binadamu (IVPP) ya Akademia ya Sayansi ya China (CAS), na kiongozi wa timu ya ufukuaji ya Hualongdong, amesema ugunduzi huo unaonyesha kuwa familia kubwa ya watu zaidi ya 20 waliishi katika eneo hilo.

"Walikuwa na 'bwalo la chakula' ambamo walikata, kukatakata vipande na kusindika vyakula. Pango la chotaa pengine lilikuwa chumba chao cha kujificha dhidi ya wanyama pori usiku, lakini limebomoka, na bado hatujalichimba. Tunatarajia kugundua visukuku vingi zaidi vya binadamu katika siku zijazo," Wu ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha