Waongoza watalii wa Ethiopia wajifunza lugha ya Kichina ili kufaidika vema na soko la watalii wa China wanaosafiri nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2024
Waongoza watalii wa Ethiopia wajifunza lugha ya Kichina ili kufaidika vema na soko la watalii wa China wanaosafiri nje
Song Ruirong, mwalimu Mchina wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, akifundisha lugha ya Kichina kwa wafanyakazi wa utalii wa Ethiopia katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia, Desemba 2, 2024.

ADDIS ABABA - Tsegaye Gebremedhin, mwongoza watalii mwenye uzoefu, ni miongoni mwa wafanyakazi 60 wa utalii wa Ethiopia wanaofaidika na nguvu ya kimageuzi ya lugha nchini Ethiopia, nchi yenye utajiri wa urithi wa kitamaduni na uzuri wa mazingira ya asili, likiweka mtazamo wake wa kufaidika na soko linalostawi la watalii wa China wanaosafiri nje.

Wakati nchi hiyo ikitafuta kuimarisha uhusiano kati ya watu, wa kiuchumi na kidiplomasia na China, kama sehemu muhimu ya mkakati wa kitaifa wa kuimarisha mchango wa sekta ya utalii katika ongezeko la uchumi wake, waongoza watalii wa Ethiopia kama vile Gebremedhin wanatambua kuwa kuifahamu vizuri Lugha ya Kichina ni mbinu muhimu wa kuongeza ujuzi wao wa kitaaluma na kuvutia watalii wa China.

Akiwa na uzoefu wa miaka 11 wa kuwa muongoza watalii, Gebremedhin ameshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watalii wa China wanaotembelea Ethiopia. Anasisitiza umuhimu wa waongozaji watalii wa Ethiopia kujifunza lugha ya Kichina ili kufaidika kikamilifu na ongezeko hilo la watalii wa China na mustakabali mzuri.

"Hapo zamani, tulikuwa tukiona raia wa China wengi wakishiriki katika sekta ya uwekezaji na ujenzi. Hata hivyo, siku hizi, tunapoenda kwenye uwanja wa ndege kukaribisha wageni wetu, idadi kubwa ya wasafiri watalii ni Wachina," Gebremedhin amesema.

Kutokana na uchunguzi wake, watalii wa China wanazidi kupenda kujionea mambo halisi nchini Ethiopia, wakiwa na shauku ya kujionea mandhari, wanyamapori na vitu mbalimbali vya urithi wa kitamaduni vya nchi hiyo. Hata hivyo, Gebremedhin anabainisha kuwa kizuizi cha lugha kimekuwa changamoto kubwa, kikiathiri hali ya jumla ya uzoefu wa watalii wa China kufanya utalii.

Kwa kutambua changamoto hiyo na mahitaji yanayoongezeka ya ujuzi wa lugha, Gebremedhin amechukua hatua za kujifunza Lugha ya Kichina. Kwa kuendeshwa na matamanio yake binafsi na fursa za kitaaluma inazotoa, amekuwa akisoma lugha hiyo kwa zaidi ya miezi sita.

"Kwa kuzungumza lugha yao na kuwaongoza kwa lugha yao ya asili, tunaweza kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya uzoefu wa watalii wa China kutalii hapa nchini Ethiopia," amesema.

Gebremedhin ni mmoja wa waongoza watalii 60 wa Ethiopia wanaojifunza lugha ya Kichina kwa sasa ikiwa ni sehemu ya mpango ulioandaliwa kutoa umahiri wa lugha ya msingi katika wiki tatu.

Mpango huo uliozinduliwa na Wizara ya Utalii ya Ethiopia kwa ushirikiano na Jumuiya ya wafanyakazi wa Waongoza Watalii wa Ethiopia (ETGPA) na Ubalozi wa China nchini Ethiopia, unalenga kuwapa wafanyakazi wa utalii na hoteli wa Ethiopia ujuzi muhimu wa lugha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha