Msimu wa kukusanya barafu waanza mjini Harbin, Kaskazini Mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 10, 2024
Msimu wa kukusanya barafu waanza mjini Harbin, Kaskazini Mashariki mwa China
Picha iliyopigwa Desemba 9, 2024 ikionyesha mfanyakazi akikusanya barafu kutoka Mto Songhua mjini Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China.

Msimu wa kukusanya barafu unapoanza mjini Harbin, vipande vya barafu vinakatwa na kuinuliwa kutoka Mto Songhua ulioganda kwa ajili ya kujenga vinyago vya barafu kwenye vivutio vya watalii katika maeneo mbalimbali ya mji huo. Moja ya vivutio hivyo vinavyojulikana zaidi ni Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin, bustani maarufu ya majira ya baridi mjini humo ambayo huvutia watalii wengi kila majira ya baridi unapowadia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha