Lugha Nyingine
China kuzidisha zaidi mageuzi kwa kina na kupanua ufunguaji mlango
BEIJING - China itafanya kazi kwa bidii zaidi kupanua mahitaji na matumizi ya ndani, kuzidisha mageuzi kwa kina, kufungua mlango zaidi, na kufanya juhudi kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa China, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema Jumapili na Jumatatu alipokutana kwa nyakati tofauti na wakuu wa mashirika ya kiuchumi ya kimataifa waliokuwa mjini Beijing kuhudhuria mazungumzo ya "1+10".
Waziri Mkuu Li alikutana kwa nyakati tofauti, na Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo Dilma Rousseff, Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva.
Kutokana na hali ya mazingira ya kimataifa iliyojaa mabadiliko na kukosekana kwa utulivu, Waziri Mkuu Li amesema, ni kwa kuimarisha tu kufungua mlango, ushirikiano na kunufaishana ndipo tunaweza kuhimiza kwa pamoja ufufukaji na ukuaji tulivu wa uchumi wa dunia.
"Mwaka huu uchumi wa China umeongezeka kwa utulivu kwa ujumla, na hivi karibuni tumetoa sera kadhaa za nyongeza. Imani na matarajio sokoni zimeimarishwa kwa kiasi kikubwa," Waziri Mkuu Li amesema, akiongeza kuwa China itafanya juhudi ili kuongeza msukumo na uhakika zaidi katika ufufukaji na ukuaji wa uchumi wa dunia.
China inaunga mkono upanuzi unaoendelea wa Benki Mpya ya Maendeleo na ingependa kupanua ushirikiano wa mradi na ukusanyaji wa fedha kati ya pande hizo mbili ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa pamoja katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi za BRICS na nchi zinazoendelea.
Amesema China ina nia ya kuimarisha ushirikiano na Benki ya Dunia katika maendeleo ya kimataifa, mikopo, ujuzi na sekta nyingine ili kuboresha sifa na ufanisi wa ushirikiano.
China inaunga mkono WTO katika kufanya mageuzi yanayohitajika, kuhimiza ustawi wa mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kulinda utandawazi wa uchumi na biashara huria, na China inapenda kuzidisha ushirikiano na IMF na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kudumisha utulivu wa mambo ya fedha duniani, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Waziri Mkuu Li amebainisha.
Kwa upande wa viongozi wa Benki Mpya ya Maendeleo, Benki ya Dunia, WTO na IMF wamezungumzia kwa kusifu sana mchango mkubwa wa China katika kulinda amani na maendeleo ya dunia na kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, wakisema China imechukua hatua na kupata matokeo makubwa katika kuhimiza ukuaji wa uchumi, kuboresha mazingira ya kibiashara na kupanua ufunguaji mlango, ikileta msukumo na imani katika ukuaji wa uchumi wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma