Migodi ya makaa ya mawe iliyotelekezwa yageuzwa kuwa“Bustani ya Maua ya Waridi” mjini Zibo, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2024
Migodi ya makaa ya mawe iliyotelekezwa yageuzwa kuwa“Bustani ya Maua ya Waridi” mjini Zibo, China
Mfanyakazi akichambua maua freshi ya waridi yaliyokatwa punde, Desemba 10. (Picha na Zhu Zheng/ Xinhua)

Katika banda la kilimo cha kisasa la Mradi Kielelezo wa Dakuishan katika eneo la Zichuan, mji wa Zibo, mkoani Shandong, China, maua ya waridi 120,000 yamechanua kikamilifu. Siku hizi wafanyakazi wanakata na kuchambua maua hayo freshi ya waridi, na kisha kuyauza katika sehemu mbalimbali kupitia majukwaa ya biashara mtandaoni.

Banda hilo la kilimo cha kisasa hutumia sifa za rasilimali za maji ya mgodi uliofungwa, ambayo ni ya vuguvugu wakati wa msimu wa baridi na ya baridi wakati msimu wa joto, ili kutumia kikamilifu vyanzo vya joto la migodi hiyo isiyofanya kazi, kudumisha joto la banda katika digrii 16 mwaka mzima, na kuunda mazingira mwafaka kwa ukuaji wa maua hayo ya waridi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha