Lugha Nyingine
Hekima ya China ya kugeuza "uyoga" kuwa dhahabu
Uyoga kuvu wa tremella ni toniki ya kijadi ya China. Ukijulikana kama "mfalme wa uyoga", uyoga huo bado ulikuwa "anasa" adimu kwenye meza katikati ya karne ya 20. Katika kipindi cha zaidi ya nusu karne, uyoga huo umekuwa wa mara kwa mara kwenye meza ya watu wa kawaida. Mageuzi haya yanahusiana kwa karibu na Gutian, mji mdogo mjini Ningde katika Mkoa wa Fujian wa China.
Hivi karibuni, Mkutano wa kwanza wa Maendeleo ya Sekta ya Uyoga Kuvu wa Tremella ulifanyika katika mji huo wa Gutian. Katikati ya mfululizo wa semina na maonyesho, "simulizi" kuhusu Uyoga Kuvu wa Tremella wa Gutian iliibuka polepole.
Katika miaka ya 1960 na 1970, uyoga huo kuvu wa Tremella ulikuwa ghali na adimu. Baadhi ya wataalam walitengeneza teknolojia ya upandaji wa kwenye magogo, na wakulima wengi wa uyoga wenye "hisia kubwa ya kunusa" waliianzisha kwa ajili ya upandaji wa majaribio.
Tangu mafanikio ya teknolojia ya kilimo mbadala cha chupa mwaka 1977, teknolojia ya upandaji uyoya kuvu wa tremella ya Gutian imepitia mabadiliko ya aina matatu. Takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa Uyoa Kuvu wa Tremella wa Gutian kwa sasa unachukua zaidi ya asilimia 90 ya nchi nzima ya China, na hata ulipandisha bei ya Tremella kwa miongo kadhaa, na kuufanya kuwa "chakula cha kawaida."
Kwa sasa, Gutian imekuwa kituo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa bidhaa za Tremella nchini China, na pia ni wilaya iliyo na msingi kamili zaidi wa uzalishaji wa uyoga kuvu unaoliwa wa aina mbalimbali.
Mauzo ya kila mwaka ya Soko la Jumla la Uyoga Kuvu Unaoliwa la Gutian mjini Fujian, China yanazidi Yuan milioni 600, na kuna kampuni zaidi ya 400 za biashara ya mtandaoni na maduka zaidi ya 2,700 ya biashara ya mtandaoni katika wilaya hiyo.
Mwaka 2023, "Uyoga Kuvu wa Tremella wa Gutian " ulishika nafasi ya pili katika orodha ya thamani ya chapa za kitaifa za uyoga kuvu unaoweza kuliwa ukiwa na thamani ya yuan bilioni 14.732, na ukashinda Tuzo Bora ya Ukuaji.
Gutian, ikiwa na "hisia kali ya kunusa", pia inachukua fursa ya kujijenga kuwa "Mji Mkuu wa Uyoga wa Tremella Duniani". Kwa sasa, mtandao wa masoko wa uyoga kuvu wa Gutian umeenea kote nchini China, na pia umeingia katika nchi na kanda kadhaa kama vile Asia Kusini Mashariki, Ulaya na Amerika, ukiwa na uzalishaji na kiasi cha mauzo ya uyoga kuvu unaoweza kuliwa cha asilimia zaidi ya 98.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma