

Lugha Nyingine
Israel yasema imeharibu asilimia zaidi ya 90 ya mifumo ya makombora dhidi ya anga ya Syria
![]() |
Moshi ukipaa kwenda angani kufuatia shambulizi la anga la Israel pembezoni mwa Damascus, Syria, Desemba 12, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua) |
JERUSALEM - Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limetangaza jana Alhamisi kuwa "limeharibu vibaya" ulinzi wa anga wa Syria, likiharibu asilimia zaidi ya 90 ya mifumo ya kimkakati ya makombora dhidi ya anga ambapo katika taarifa yake, IDF imesema kuwa imefanya tathmini ya kina kwa hali ya Syria, ikitilia maanani uwezekano wa kuanguka kwa Bashar al-Assad.
"Ili kukabiliana na hali kama hiyo, Jeshi la Anga limeandaa mpango mkubwa wa mashambulizi unaolenga kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Syria, zikiwemo silaha za kimkakati," imesema taarifa hiyo.
Katika siku kadhaa zilizopita, mamia ya ndege na vyombo vya kivita vya angani vya Israel vimekuwa vikianzisha mashambulizi, yakitoa pigo kubwa kwa silaha za kimkakati za Syria, zikiwemo ndege za kivita, helikopta, makombora, UAV, rada na roketi.
Mashambulizi hayo pia yamelenga vituo kadhaa muhimu vya anga nchini Syria. Uwanja wa ndege wa T4, karibu na sehemu ya kaskazini ya Damascus, umeharibiwa kwa kiasi kikubwa, huku kukiwa na uharibifu kamili wa ndege za kivita za SU-22 na SU-24 zilizokuwa zimewekwa hapo. Uwanja wa ndege wa "Ble", uliokuwa ukihifadhi ndege tatu nyingine za kivita, na ghala la karibu la silaha pia umepigwa na mashambulizi hayo ya Israel.
Aidha, miundombinu ya utengenezaji na uhifadhi, ikijumuisha mmoja wa muhimu katika eneo la Homs nchini Syria, ambao ulithibitishwa kuwa sehemu muhimu ya mpango wa makombora wa Scud wa Syria, imelengwa.
Taarifa hiyo ya IDF imeonyesha kuwa operesheni hizo zililenga kushusha chini uwezo wa hali ya juu wa kijeshi wa Syria huku kukiwa na mvutano unaoongezeka katika eneo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma