Kampuni zinazowekezwa na Wachina zafanya vyema katika kutimiza wajibu wa kijamii nchini Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2024
Kampuni zinazowekezwa na Wachina zafanya vyema katika kutimiza wajibu wa kijamii nchini Afrika Kusini
Balozi wa China nchini Afrika Kusini Wu Peng akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti yenye jina la "Ripoti ya CSR Mwaka 2024 ya Kampuni Zinazowekezwa na Wachina nchini Afrika Kusini" mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Dec. 11, 2024. (Xinhua/Zhang Yudong)

JOHANNESBURG – Kampuni zinazowekezwa na Wachina nchini Afrika Kusini zimetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo huku zikifanya vyema katika uwajibikaji wa kijamii wa kampuni za kibiashara (CSR), kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatano na Jumuiya ya Uchumi na Biashara ya Afrika Kusini na China (SACETA).

Ripoti hiyo ya CSR Mwaka 2024 ya Kampuni Zinazowekezwa na Wachina nchini Afrika Kusini, toleo la pili kufuatia kuchapishwa kwake kwa mara ya kwanza Mwaka 2018, inaonyesha mafanikio yao makubwa katika kutimiza wajibu wa kijamii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kupitia utafiti mbalimbali wa kina na picha zinazoonyesha hali halisi.

Hadi sasa, kampuni zaidi ya 200 zinazowekezwa na Wachina zinafanya kazi nchini Afrika Kusini. Ripoti hiyo inaangazia mchango wao katika kuendeleza "msukumo mpya wa uwekezaji" wa Afrika Kusini na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika sekta kama vile nishati mpya, viwanda, madini na uchumi wa kidijitali, zikiingiza nguvu mpya katika sekta za kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo.

Ripoti hiyo inasisitiza dhamira ya kampuni hizo za China katika huduma za kijamii, ulinzi wa mazingira, maendeleo ya wafanyakazi, na mawasiliano ya kitamaduni, ambayo yamezifanya kusifiwa sana na serikali za mitaa na jamii.

Balozi wa China nchini Afrika Kusini Wu Peng amesema kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo kwamba inaangazia mchango mkubwa unaotolewa na kampuni hizo za China kwa maendeleo ya Afrika Kusini. Mchango huo unahusisha sekta kama vile kuboresha maisha ya watu, kulinda mazingira, na kuunga mkono sekta mbalimbali.

"Hii inaonyesha vizuri namna kampuni za China zinavyotekeleza kwa uaminifu kanuni ya udhati, ukweli, upendo, na nia njema, na kuchukua njia sahihi ya urafiki na maslahi," amesema Wu.

Makamu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile ambaye pia alizungumza kwenye hafla hiyo, amepongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, akibainisha dhamira yao ya pamoja ya maendeleo endelevu na usimamizi wa kampuni.

"Ripoti inayozinduliwa leo inaangazia mchango wa kampuni zinazowekezwa na Wachina nchini Afrika Kusini katika uhifadhi wa mazingira, maendeleo ya jamii, elimu na huduma za afya," Mashatile amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha