Walimu 80 wa lugha ya Kichina washiriki kwenye warsha ya kuboresha ujuzi wa kufundisha nchini Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2024
Walimu 80 wa lugha ya Kichina washiriki kwenye warsha ya kuboresha ujuzi wa kufundisha nchini Tanzania
Aldin Mutembei, Mkurugenzi wa Tanzania wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa warsha kwenye Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, Desemba 14, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM- Walimu takriban 80 wa lugha ya Kichina kutoka Tanzania na China wameshiriki kwenye warsha ya siku mbili kwenye Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania kwa lengo la kuboresha ujuzi na maarifa yao ya kufundisha.

Warsha hiyo ya siku mbili imeshirikishwa na walimu kutoka China, Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Darasa la Confucius la Chuo Kikuu cha Serikali ya Zanzibar, Taasisi ya Elimu Tanzania, Taasisi ya SAY ya Zanzibar, na shule za msingi na sekondari kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Mkurugenzi wa Tanzania wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Aldin Mutembei, amesema warsha hiyo inatoa fursa ya kipekee ya kuongeza maarifa na ujuzi wa kitaalamu unaoboresha uzoefu wa wanafunzi kujifunza.

Mutembei amesema ufundishaji lugha ya Kichina nchini Tanzania na kote barani Afrika umekuwa muhimu siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kiutamaduni kati ya China na Afrika, akiongeza kuwa kujua lugha ya Kichina kunaweza kuimarisha zaidi uhusiano kati ya watu na watu, ikiwezesha Watanzania kuwasiliana na kushirikiana kwa ufanisi zaidi na watu wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha