Luteni Jenerali wa Jeshi la Russia na msaidizi wake wauawa katika mlipuko wa mjini Moscow

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2024
Luteni Jenerali wa Jeshi la Russia na msaidizi wake wauawa katika mlipuko wa mjini Moscow
Picha hii iliyopigwa Desemba 17, 2024 ikionyesha eneo la mlipuko mjini Moscow, Russia. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua)

MOSCOW - Luteni Jenerali wa Russia Igor Kirillov, ambaye pia ni mkuu wa vikosi vya ulinzi wa kiradiolojia, kikemikali na kibiolojia vya Jeshi la Russia na msaidizi wake wameuawa kwenye mlipuko uliotokea katika jengo la makazi mjini Moscow jana Jumanne asubuhi, imesema Kamati ya Uchunguzi ya Russia.

Habari zilizopatikana awali zinasema kuwa mlipuko huo umetokea baada ya kulipuka kwa kifaa kilipuko, ambacho kilikuwa na nguvu ya gramu takriban 200 za TNT.

Kifaa hicho cha kulipuka kiliwekwa kwenye pikipiki, imesema kamati hiyo, ikiongeza kuwa kesi ya jinai kuhusu mauaji hayo imefunguliwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha