Katika Picha: Walinzi wa Mlima Huangshan, Eneo la Urithi wa Dunia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2024
Katika Picha: Walinzi wa Mlima Huangshan, Eneo la Urithi wa Dunia
Hu Xiaochun (kulia), mfanyakazi anayeshughulikia utunzaji wa kila siku wa Msonobari wa Kukaribisha Mgeni, ambao ni mti maarufu katika Mlima Huangshan, akizungumza na Wu Yijun, mhandisi mwandamizi katika ofisi ya hifadhi na misitu ya kamati ya usimamizi wa Eneo la Kivutio cha Watalii la Huangshan kuhusu hali ya msonobari huo, katika Eneo la Kivutio cha Watalii la Huangshan, Mkoani Anhui, mashariki mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Fu Tian)

Mlima Huangshan katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China ni Eneo lililoorodheshwa kwenye orodha ya Urithi wa Kitamaduni na Mazingira ya Asili wa Dunia wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na uhifadhi wa mandhari, misitu na maandishi yake ya miamba imekuwa matumaini na dhamira ya pamoja ya watu wengi.

Kutokana na juhudi kubwa za walinzi kutoka makundi yote ya kijamii, Mlima huo Huangshan umeendelea kuwa onyesho la kuvutia la uzuri wa ikolojia na urithi wa kitamaduni kwa mapatano ya hali ya juu, ukivutia watalii kutoka kote duniani. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha